Filamu Mpya ya Cultural Wars Sasa Yapatikana! Wahi Kujipatia DVD! |
Ile filamu mliyokuwa mnaisubiri kwa hamu iitwayo “Cultural Wars”
iliyoandikwa na kutengenezwa na Deogratius Mhella (Mtanzania anayeishi
New York) akishirikiriana na Watanzania na Wamarekani waishio New York,
New Jersey Boston na Connecticut sasa imetoka kwa mara ya kwanza na
inapatikana kwenye DVD na unaweza kupata “electronic Copy”
Filamu hii inazungumzia baadhi ya changamoto za kimapenzi wazipatazo
vijana wa Kitanzania hapa Marekani. Na ni ya kwanza iliyochezwa na
Watanzania na Wamarekani hapa New York kwa kutumia lugha ya Kiingereza.
Baadhi ya “Actors” wa Kitanzania ni Khalifa Siwa aka “Bob”, Ny Ebra
aka “Vijimambo New York”, Akida aka “Mshenga”, Chemi Whitlow aka
“Chemponda” na Isaac Kibodya aka “Father”. Wote mliosaidia katika
kufanikisha filamu hii ambao hamjatajwa hapo juu, mnapewa shukrani za
dhati kabisa.
Usikose kujipatia nakala yako kwa kuinunua au kuiona kupitia link hapa chini:
0 comments:
Post a Comment